Search
Sunday, November 3, 2013
Kuhusu mauaji yaliyotokea Marekani kwenye hiki kiwanja cha ndege
Mtu mmoja ameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa saa tatu asubuhi baada ya mtu mmoja kuingia na bastola kwenye uwanja wa ndege wa Las Angeles na kufyetua risasi ovyo ambazo zilijeruhi na kuua mfanyakazi mmoja ndani ya uwanja huu wa ndege sehemu ya Terminal 3.
Kwa mujibu wa gazeti la The Gurdian, mtuhumiwa huyu aitwae Paul Ciancia mwenye umri wa miaka 23, alipigwa risasi mara nne na polisi waliokuwepo Airport zilizopelekea kulazwa hospitali mpaka sasa huku akisubiri mkono wa sheria kufanya kazi yake.
Ujumbe uliokutwa ndani ya begi la Paul ambae hana rekodi ya uhalifu, umesema alikua amepanga kumuua mwajiriwa wa TSA ambao wanahusika na usalama kwenye viwanja vya ndege vya Marekani pamoja na Nguruwe kwenye shambulio hilo ambalo baada ya kutokea, lilisababisha usumbufu kwa ndege zaidi ya 700 ambazo zilikua kwenye safari inayohusu uwanja huu.
Risasi hizi ambazo zilipigwa kwenye sehemu watu wanapotumia kupita na kuchek mizigo kabla ya kusafiri, zilisababisha usumbufu kwenye dakika hizo kabla ya mtuhumiwa kukamatwa ikiwemo watu kukimbia na kupiga kelele za kuomba msahama.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment